BRENDAN
Rodgers amepewa ofa nzuri ya kazi katika klabu ya Liverpool kwa kusaini mkataba
mwingine utakaomfanya akae muda mrefu zaidi Anfield.
Rodgers,
aliyebakiwa na miezi 12 katika klabu hiyo amepewa zawadi hiyo ya mkataba baada
ya kufanya vizuri ligi kuu na sasa amemwaga wino katika mkataba mpya
unaosemekana kumuweka Merseyside mpaka 2018.
Liverpool
walimaliza pointi mbili tu nyuma ya mabingwa Man City tangu mwaka 1990 na
walionesha kiwango kikubwa mno chini ya Rodgers na kuwavutia Wamiliki wa klabu
hiyo, raia wa Marekani.
Tangu
Rodgers ajiunge na Liverpool 2012 akitokea Swansea City amekuwa kivutio kwa
mashabiki na wamiliki wa klabu hiyo na sasa wanajiandaa kumpa dau la kutosha
kufanya usajili kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya UEFA.
No comments:
Post a Comment