Waombolezaji wakitoa heshima zao huku wengine wakichukua picha za kumbukumbu |
Mhubiri aliyejitolea baada ya kanisa la Rc kususa kuendesha misa |
Marehemu enzi za uhai wake |
Kijana wa boda boda akifurahia kuwapokonya chepe wenzake |
Vijana wakizichapa ngumi kugombea kuzika |
Mwenyeji walikuwa watazamaji baada ya boda boda kuchukua jukumu zima la kuzika katikati ni mwenyekiti wa waganga wa tiba asilia mkoa wa Iringa Galusi Msekwa |
……………………………………..
Na www.mwandishiwetu.blogspot.com
MATUMAINI ya vijana dhidi ya chama demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Iringa mjini imeanza kutoweka baada ya jana dereva boda boda zaidi ya 200 kuwazuia viongozi wa Chadema kupeperusha wala kufunika bendera za chama hicho katika bajaji iliyobeba mwili wa dereva mwenzao Abisai Mdesa .
Vuta nikuvute hiyo ilitokea majira ya saa 4 asubuhi baada ya makada wa Chadema kufika Chumba cha maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa wakiwa na bendera za Chadema kwa ajili ya kuwapa madereva wa boda boda pamoja na kufunga katika bajaji iliyopaswa kubeba mwili wa marehemu huyo bado bado msimamo wa boda bado ulionekana kupingana na matakwa ya viongozi hao.
Vijana hao walionesha kupinga msimamo wa makada hao wa Chadema kutoka kufunika bendera wa chama chao katika jeneza la marehemu huyo wala kupeperusha bendera ya chama chao katika msafara wa mazishi kwa madai kuwa chama hicho cha boda boda Iringa si chama cha kisiasa na wala hakina ubia na Chadema .
Wakizungumza kwa jazba vijana hao waendesha boda boda boda walisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha Chadema kutaka kujipatia umaarufu kupitia mazishi ya dereva mwenzao huyu hali wakitambua kuwa wao si sehemu ya Chadema.
Walisema walikuwa tayari kuwashambulia kwa kipigo makada hao wanne wa Chadema waliofika na bendera hizo iwapo wangeshindwa kuwasikiliza na kuendelea na msimamo wao wa kufunga bendera.
Mwenyekiti wa chama cha boda boda na Bajaji mjini Iringa Joseph Mwambope aliwaeleza waandishi wa habari kuwa hatua ya Chadema kutaka kujimilikisha msiba huo ni kosa kubwa na kuwa wanachotambua kuwa marehemu hakuwa kiongozi wa Chadema ila alikuwa ni mwanachama wa chama cha boda boda hivyo mbali ya ndugu mwenye nafasi ya kuendesha mazishi hayo ni chama cha boda boda na Bajaji pamoja na wasanii wenzake wa Mundu Sanaa Group na sio chama chochote cha siasa.
“Tunaomba ieleweke kuwa chama cha boda boda si chama cha kisiasa hivyo haturuhusu Chadema ama CCM kuja na bendera za vyama vyao katika msiba huu japo hatuwakatazi kuja na magari yao yakiwa na bendera za vyama vyao ila sio kuleta bendera tufungi kwenye boda boda na bajaji zetu “alisema Mwambope
Kuwa imekuwa ni kawaida ya Chadema na vyama vingine kujipendekeza katika misiba ambayo wanahisi ina waombolezaji wengi ili kutumia nafasi hiyo kujitangaza kisiasa ila wakati wa kuuguza vyama hivyo huwa havitokei kuuguza.
” Huyu mwenzetu mbali ya kupata ajali ya pikipiki kwa siku zaidi ya nne sasa alikuwa amelezwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na madereva tulianza kuchangishana ili kumfanyia rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili …..sasa kama Chadema ambao leo wanakuja na bendera wapo kwanini wasingetoa usafiri wa kwenda Muhimbili kama si kutaka kuonekana sasa baada ya kifo”
Katika hatua nyingine vijana hao wa boda boda walilazimika kuzomea kada wa Chadema aliyepewa kuweka shada kaburini kutokana na kushindwa kukabidhi ahadi yao ya mchango wa shilingi 25000 ambazo waliahidi kwenye daftari la waombolezaji bila kutoa pesa hiyo .
Kijana huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mpenzi wa Chadema ambae mara kadhaa alionekana kupanda juu ya miti mirefu na kufunga bendera za Chadema .
No comments:
Post a Comment