Pages

Wednesday, May 21, 2014

Hosni Mubarak jela miaka 3



Hosni Mubarak wakati kesi yake ilipokuwa inaendelea
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Hosni Mubarak amehukumiwa jela miaka mitatu.
Wanawe wawili Alaa na Gamal wamepata kifungo cha miaka minne kila mmoja.
Wendesha mashitaka walisema kuwa wanawe Mubarak waliponda mamilioni ya dola pesa za umma zilizotengewa kukarabati ikulu ya Rais na badala yake wakafanyia ukarabati nyumba zao za kifahari.
Wametakiwa kulipa pesa hizo za serikali na kutozwa faini ya dola milioni tatu.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment