Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limelazimika
kuwaita wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) wa Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro kushuhudia mwili wa mtu aliyekutwa amekufa kwenye kichaka
jirani na ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.
Kwa
mujibu wa polisi, mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Juma Mbega (46)
ulikutwa kwenye kichaka ukiwa umeharibika vibaya na kutoa harufu kali huku
ukizungukwa na wadudu, nusura polisi wenyewe watoke nduki.
Akizungumza
na mwanahabari wetu, Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Afande
Suzy alisema wakiwa ofisini, walisikia harufu kali hivyo kulazimika kufanya
uchunguzi ndani na nje ya jengo hilo la polisi lenye ghorofa moja ambapo chini
zipo ofisi za Jeshi la Polisi Wilaya ya Morogoro Mjini na juu za mkoa. Baada ya
kuchunguza harufu hiyo, tulibaini uwepo wa maiti kwenye kichaka kilichopo nje
ya ofisi zetu ambapo mwili huo unaokadiriwa kuwepo hapo kwa zaidi ya wiki moja
ulikuwa umeharibika vibaya na kutoa harufu kali
alisema
afisa huyo.
Kwa
upande wake, Nuru Adam ambaye ni mjomba wa marehemu huyo, akizungumza na gazeti
hili eneo hilo la tukio alisema: Huyu ni mjomba’ngu, amezaliwa tumbo moja na
mama yangu mzazi, Kilegu Hamis.
Alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka hivyo huenda alikutwa na matatizo hayo
akiwa eneo hili peke yake.Baada ya uchunguzi wa awali na ndugu wa marehemu
kujulikana, maiti ilichukuliwa na kupelekwa mochwari kuhifadhiwa huku taratibu
za mazishi kwa ndugu zikiendelea.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo.picha na GPL
No comments:
Post a Comment