skip to main |
skip to sidebar
HUZUNIII:::PICHA ZA KICHANGA KILICHOTUPWA MTO MWANANYAMALA
Wakazi wa Mwananyamala wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI
wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa
eneo la mto Ng'ombe jirani na Rasco, Mwananyamala jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo.
Mtandao
huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi.
Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo
viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango
kujikinga na matatizo kama hayo.
"Nina masikitiko makubwa kwa
kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko
kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi
wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina
kumtafuta muhusika!
-GPL
No comments:
Post a Comment