Pages

Tuesday, May 6, 2014

JE UNA MAONI GANI KWA MANENO HAYA ALIYOKUWA ANATUMIA MSANII MPOKI KWENYE TUZO ZA KILI 2014


Slivery Mujuni, ‘Mpoki’ (mwenye kipaza sauti) aliyekuwa mshereheshaji katika KTMA2014. Usiku wa Jumamosi ulikuwa ni usiku mkubwa zaidi wa mwaka huu kwa wanamuziki na labda muziki wa Tanzania. Ulikuwa ni usiku wa tuzo za muziki na wanamuziki bora nchini Tanzania.
Tamasha lenyewe lilifanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na lilishirikisha wanamuziki, wadau wa muziki na wageni mbali mbali kutoka kote ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Moja ya zilizo kuwa nguzo za usiku huo ni msherekesha wa shughuli aka ‘MC’, nafasi aliyopewa Bw. Silvery Mujuni aka ‘Mpoki’.
Hakuna ubishi kuwa Bw. Mpoki ana uwezo mkubwa, kitu kinachothibitishwa na mafanikio yake mwenyewe na yale ya kundi lililompa umaarufu la ‘Ze Komedi’.
Lakini kwa usiku ule, Mpoki alionekana ‘kutokuiva’ kwa shughuli aliyopewa. Shughuli aliyopewa ilikuwa ni ya Kimataifa, kitu ambacho ndugu huyo huenda kwa kiasi fulani alishindwa kutambua na akabaki kuiendesha kama tulivyozoea kuona harusi za ‘kiswaili’.
Ndugu Mpoki ni mchekeshaji, lakini alishindwa kupima utani wake kitu ambacho kilionekana kuwaudhi labda hata kuwadhalilisha baadhi ya washiriki wa KTMA2014.
Kwa mfano mara kadha alionekana kulikazia swala la viatu virefu vya kike (high heels) na kuwakumbusha akina dada mara kwa mara, ‘kuvifanyia mazoezi’.



Pia Mpoki alimtupia Martin Kadinda, Meneja wa Wema Sepetu muigizaji maarufu maneno ambayo yaliyoonekana kumuudhi hadi Meneja huyo akamjibu kistaarabu alivyoweza ingawa ilikuwa dhahiri kuwa maneno ya Mpoki hayakumfurahisha.
Muimbaji Vanessa Mdee naye alikuwa mmoja ya wale ‘waliotaniwa’ na Mpoki. ‘Alitaniwa’ kwa kuwa baada ya kupokea tuzo alizungumza maneno fulani, na kusema ukweli akajigamba kidogo, huku akichanganya lugha ya Kiswaili na Kiingereza, Mpoki alimtupia maneno ambayo hayawezi kuwa si kashfa.
Hata ‘Shadee’ msherekeshaji mwenzake na Mpoki alionekana kutokuwa ‘ukurasa mmoja’ na Mpoki mara kadha.
Nimejaribu kuweka baadhi tu ya vitu nilivyoona si sawa. Au mimi ndiye mshamba?

1 comment: