Tangu Nemanja
Vidic alipotangaza rasmi kwamba msimu ujao hatokuwepo Old Trafford
kulianza tetesi juu ya mchezaji gani atapewa nafasi ya kurithi mikoba ya
unahodha ambapo Wayne Rooney mmoja wa wachezaji wakubwa ndani ya klabu
ya Manchester United alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha mpya
wa United wakati timu hiyo ikiwa chini ya David Moyes.
Baada
ya kutimuliwa kwa kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Louis Van
Gaal, mshambuliaji wa Uholanzi na nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi
Robin van Persie amekuwa akipewa nafasi ya kumrithi Vidic, huku Van Gaal
akisema kwamba yeye na RVP wana filosofia moja hivyo wanakuwa na
urahisi wa kufanya kazi pamoja kama kocha na nahodha wake.
Hali
hiyo imepelekea Wayne Rooney ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya
unahodha msimu ujao kuzungumza akisema “navutiwa na suala la kuwa
nahodha, nimeshawahi kuwa anahodha wa muda United kwa mara kadhaa na kupata jukumu hilo moja kwa moja litakuwa jambo zuri sana.”Akizungumzia suala la Van Persie kupewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha ajaye wa United, Rooney anakwambia ikiwa kocha wetu atamchagua mtu mwingine basi kiukweli kabisa sitokuwa na tatizo na hilo, nitaheshimu maamuzi yake… Robin
ni nahodha wa nchi yake, ameshawahi kuwa nahodha wa Arsenal na ikiwa
atapata nafasi hiyo United basi naamini atafanya kazi nzuri.”
No comments:
Post a Comment