Pages

Monday, May 5, 2014

KIJANA WA MIAKA 15 AFA MAJI WAKATI AKIOGELEA BWAWANI NA WENZAKE

Mtu mmoja Mkazi wa mtaa Shunu kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga, aliyejulikana kwa jina la Frank Fred mwenye umri wa miaka 15, amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye kwenye Bwawa.  



Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni wakati marehemu Frank akiogelea na wenzake katika Bwawa hilo lililopo maeneo ya KTM wilayani Kahama, ambapo alizama kusababisha kifo chake. 

Mwili wa Marehemu Frank umefanikiwa kutolewa leo majira ya saa nne asubuhi, ukiwa chini ya kina kirefu katika bwawa hilo, mara baada ya hapo jana wazamiaji mbalimbali kuhangaika kuutafuta bila mafanikio yoyote.
Vijana waliozamia na kufanikisha kuupata mwili wa Marehemu wakiwa pembeni ya mwili huo

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mifugo, alifika katika bwawa hilo akiwa na Panga ambalo inasemekana alitumwa na mwajiri wake kukata majini kwa ajili ya kulisha mifugo hiyo.




Kwa mujibu wa Wachungaji wenzake, Marehemu Frank mara kwa mara amekuwa akiwatizama wenzake wakiogelea huku yeye akiogopa, lakini jana aliamua kuogelea kwa lengo la kujifunza kuogelea kama wenzake. 





Akizungumza Muuguzi mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Richard Mabagala amethibisha kupokea mwili wa marehemu leo asubuhi, na kwamba umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Mwili wa Marehemu Frank uhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama

Jeshi la polisi wilaya ya kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taratibu za Mazishi zinafanywa na Wazazi wa Marehemu ambao ni wakazi wa Busenda kata ya Kilago wilayani humo.

No comments:

Post a Comment