Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 4, 2014

LIGI KUU ENGLAND : MAN UNITED YAPIGWA 1-0 NASUNDERLAND

Wachezaji wa Manchester United wakisikitika baada ya kipigo leo 
GUNDU bado lipo Manchester United licha ya kubadilisha kocha, baada ya jioni hii kufungwa bao 1-0 na Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Kipigo hicho katika mchezo wa pili wa Ryan Giggs tangu arithi mikoba ya David Moyes, kinaipa ahueni Sunderland na kuipeusha kwenye balaa la kushuka daraja.
Lilikuwa ni bao pekee la Sebastian Larsson dakika ya 30 ambalo leo hii limeirejesha Man United katika zama za vipigo chini ya Moyes, huo ukiwa ushindi wa kwanza wa Sunderland Uwanja wa Old Trafford tangu mwaka 1968.
Sebastian Larsson akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la ushindi Sunderland
Makocha wapya, gundu pale pale: Kocha Mkuu, Ryan Giggs na wasaidizi wake Nicky Butt na Paul Scholes leo

No comments:

Post a Comment