Glen Johnson amewajia juu mashabiki wanaomponda kwamba alicheza hovyo katika safu ya ulinzi na kuwaruhusu Crystal Palace kusawazisha mabao yote matatu na kulazimisha sare ya 3-3 katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Matokeo hayo yameifanya Liverpool ipoteze matumaini ya kutwaa ubingwa na sasa inaomba muujiza utokee kwa wapinzani wao Man City kupoteza mechi zao.
Liverpool waliongoza kwa mabao 3-0 mpaka dakika ya 79 kwenye uwanja wa Selhurst Park, lakini Palace ndani ya dakika 10 walisawazisha mabao yote.
Bao la kusawaisha la Damian Delaney na mawili ya Dwight Gayle yalimfanya Luis Suarez amwage machozi jana, lakini hali ya Johnson ilikuwa mbaya zaidi baada ya kulia mno.
No comments:
Post a Comment