Serikali ya Malaysia, imetoa data
iliyotumika kuthibitisha kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka MH370 ilianguka
kusini mwa bara Hindi.
Data hiyo ilitolewa kwanza kwa jamaa
wa abiria wa ndege hiyo ambao wamekuwa wakitaka maafisa wakuu kutoficha taarifa
zozote kabla ya vyombo vya habari kutoa taarifa hiyo.
Data hiyo iliyotolewa Jumanne,ni ya
kurasa 47 pamoja na maelezo mengine kutoka kwa kampuni ya uingereza ya
Inmarsat.
Ndege ya MH370 ilitoweka tarehe 8
mwezi Machi, ilipokuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Ilikuwa imewabeba watu 239 wengi
wakiwa raia wa Uchina.
Tangu kupotea , ndege hiyo
haijaonekana na hakuna sababu iliyotolewa ya kupotea kwa ndege yenyewe.
Data iliyotolewa inaonyesha
mawasiliano ya kawaida kati ya marubani na na mtambo wa Satelite ambayo
yaliwasababisha wachunguzi kufikia kuwa ndege hiyo ilimaliza safari yake nchini
Australia.
Wakati huohuo, msako wa chini ya
bahari kuitafuta ndege hiyo kwa kutumia Manowari ya Roboti, bado unaendelea
mjini Perth, Australia.
|
No comments:
Post a Comment