Pages

Saturday, May 17, 2014

Man Utd ilipata faida kubwa msimu huu





Manchester Utd ilipata faida kubwa licha ya kushindwa uwanjani.
Timu ya Manchester United imeripoti faida ya asilimia 20 katika kipindi cha msimu huu ambao haikunawiri uwanjani .
Katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa msimu huu The Red Devils walisajili faida ya pauni milioni 11 ikilinganishwa pauni milioni 3.6m iliyopata mwaka tangulia.
Aidha timu hiyo ilipata jumla ya pauni milioni 115.5 katika msimu uliopita asilimia kubwa ya faida hiyo ikipatikana kutoka kwa mauzo haki ya upeperushaji matangazo na mapato kutokana na tiketi za mechi.
Timu hiyo inasemekana imeandikisha mkataba wa miaka mitatu na kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anayetarajiwa kuchukua pahala pa David Moyes,aliyetimuliwa mwisho wa mwezi uliopita kufuatia msururu wa matokeo duni.
Tangazo rasmi litatolewa juma lijalo baada ya Kocha huyo kukamilisha maandalizi ya mechi ya kujipima nguvu dhidi ya timu ya Equador.

Louis van Gaal anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha kwa miaka 3
Naibu mwenyekiti wa klabu hicho Ed Woodward aliwaambia wenye hisa wa klabu kuwa klabu hiyo imesajili faida ya zaidi ya asilimia 20% na kuiweka katika nafasi nzuri ya kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Ed Woodward,kaimu mwenyekiti Man Utd

" ''mnajua hatukufanya vyema msimu uliopita na tulimaliza katika nafasi ya 7 nje ya mshindano yeyote ya bara Uropa kwa hivyo hatuna budi kununua wachezaji ilikuimarisha uwezo wa timu yetu katika msimu ujao'."
Asilimia kubwa ya faida hiyo (£42.8m) ilitokana na kuimarika kwa malipo ya udhamini kutokana na kandarasi iliyotiwa sahihi na kampuni za Aperol na Eurofood iliyoko Asia kusini.
Mapato kutokana na hati ya upeperushaji wa mechi za timu hiyo yaliimarika kwa asili mia 64 ama pauni milioni 35.6m ilihali faida iliyotokana na uuzaji wa tiketi za mechi ilileta pauni milioni £37.1m.
Kutokana na faida hiyo kubwa Manchester united ilipunguza deni lake kwa takriban pauni milioni 16 na sasa deni lililosalia ni pauni milioni £351.7m.
Kulingana na kampuni ya uhasibu ya Deloitte Football Money League, Manchester United inaorodheshwa ya nne bora miongoni mwa vilabu tajiri zaidi duniani.
Hisa zaklabu hiyo zilianza kuuzwa kwenye soko la hisa la New York Stock Exchange mwaka wa 2012 .

No comments:

Post a Comment