Pages

Tuesday, May 27, 2014

MBEYA CITY FC YAKUBALI KIPIGO CHA 2-1 KUTOKA KWA AFC LEOPARD MJINI KHARTOUM



kutoka mjini Khartoum nchini Sudan  wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi wamefungwa mabao 2-1 na AFC Leopard ya Kenya katika mchezo uliopigwa kuanzia majira ya saa 2:00 kamili usiku mjini Khartoum.
Bao la Mbeya City fc limefungwa na kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke.
Hata hivyo inaelezwa kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri kwa timu zote, lakini AFC walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza.
Ushindi huo unawafanya AFC Leopard wakae kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha pointi 6.

No comments:

Post a Comment