Timu ya Mbeya City, yenye maskani yake jijini Mbeya Tanzania, imepata bahati ya kushiriki mashindano ya CECAFA Nile Basine Cup, yatakayoanza nchini Sudan May 22, mwaka huu.
Hiyo itakuwa ni bahati ya aina yake kwa timu hiyo iliyoibukia hivi
karibuni na kushika nafasi ya tatu katika ligi iliyofikia ukingoni,
ambapo Azam wao walifanikiwa kunyakua ubingwa wa Bara.
Akizungumza jijini Mbeya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Nicolas Musonye, alisema kuwa
timu hiyo itafanikiwa kushiriki mashindano hayo mwaka huu.
Alisema kuingia katika mashindano hayo kwa Mbeya City ni sehemu ya
kuiweka sawa timu hiyo iliyoibukia hivi karibuni ikiwa na ndoto nyingi.
Tumepanga timu ya Mbeya City iweze kushiriki mashindano haya makubwa kwa mwaka huu, tukiamini ni sehemu ya kukuza soka la Afrika kwa ujumla wake
alisema.
Musonye leo alikuwa mjini Mbeya kwa ajili ya ukaguzi wa Uwanja wa
Sokoine, uliopo hapa, ambapo alipata fursa ya kutembelea na kuzungumza
na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment