Moto Uliozuka Hospitalini wauwa watu
21 Nchini Korea Kusini.Wagonjwa wapatao 20 pamoja muuguzi wameuawawa baada ya
moto mkubwa kuwaka hospitalini katika jimbo la Janseong nchini Korea Kusini,
huku wengine 6 wakiwa hali mahututi baada ya moto huo katika hospitali ya
Hyosarang iliyoko kilomita 300 kusini mwa Seoul.
Wengi wa walioaga dunia wanafikiriwa
kuwa wazee wenye umri wa kati ya miaka 70 na 80 na wasioweza kutembea.Maafisa
walisema kuwa wengi waliokufa walikosa hewa kutokana na gesi zenye sumu.Moto
huo ulizimwa kwa takribani nusu saa.
Moto huo ulianza muda mfupi tu baada
ya saa sita usiku katika hilo jumba lenye orofa tatu.Vyombo vya habari
vinaarifu kuwa wengi wa wagonjwa waliokuwa katika orofa ya juu ya jumba hilo
walishindwa kujiokoa kwa sababu vyuba vyao vilikuwa vimejaa moshi uliotokana na
moto huo.
Muuguzi huyo aliyekufa alikuwa
akijaribu kuzima moto kwa kutumia kizima moto kulingana na shirika la
Agence-France Presse.Ripoti ya shirika la Yonhap ilisema kuwa polisi walisema
kuwa jumba hilo lilikuwa limefanyiwa uchunguzi wa kiusalama majuzi.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Lee
Hyung Seok aliomba msamaha na kuwaambia wanahabari kuwa alikuwa ametenda dhambi
kubwa, na kuwa hangetoa visababu wakati watu wameaga dunia.
Tukio hili limekuja wakati wananchi
wa Korea kusini wakiendelea kuomboleza vifo vya zaidi ya watu 300 waliofariki
katika ajali ya feri iliyotokea mwezi uliopita.Rais wa taifa hilo Park
Geung-Hye ameliomba taifa radhi kirasmi kwa ajali hiyo ya feri, huku akiahidi
kuimarisha viwango vya usalama.Waziri mkuu Chung Hong-won wakati huo alijiuzulu
kwa madai ya jinsi serikali ilivyokuwa ikikabiliana na majanga.
Ajali hiyo ya hospitali pia imetokea
siku moja tu baada ya watu 7 kuuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mkasa wa
moto uliozuka katika kituo cha mabasi jijini Goyang.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment