Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSANII wa filamu hapa nchini, Adam Kuambiana, pichani juu, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa Jumanne katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku mazishi yake yakitanguliwa na shughuli ya kumuaga katika Viwanja vya Leaders Club, saa 2 kamili asubuhi.
Akizungumza leo mchana, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Maafa na Sherehe wa Chama Cha Waigizaji mkoani Dar es Salaam, Kaftany Masoud, alisema taratibu za mazishi yake zitaanza kwa kuagwa Leaders Club.
Katika hatua nyingine, msanii wa maigizo na filamu, anayejulikana kwa jina la Ridhiwan Masoud, amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, hivyo kuendeleza wimbi la misiba ya wasanii na wanamuziki Tanzania, ukiwamo msiba wa Amina Ngaluma, mwanamuziki wa dansi, ambaye jumanne na Jumatano mwili wake utaletwa Tanzania tayari kwa masishi yake.
Msiba wa msanii huyo upo maeneo ya Magomeni Mapipa, mtaa wa Mkadini, ambapo ndipo zitakavyoendelea taratibu za mazishi yake.
No comments:
Post a Comment