Nahodha na wafanyakazi wengine
watatu wa feri iliyozama katika ufuo wa Bahari Korea Kusini mwezi
uliopita wameshitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Wanashitakiwa kwa kuondoka kwenye feri hiyo,
ijulikanayo kama Sewol, huku wakiwambia abiria wao kuwa wasiondoke
katika chombo hicho.Wafanyakazi wengine 11 wa meli hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazini.
Zaidi ya abiria 280 - wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule ya upili karibu na Seoul - walikufa maji wakati feri hiyo ilipozama.ChanzoBBC
No comments:
Post a Comment