Mwili wq ‘janki’ Geoffrey Mlelwa ukiwa kwenye gari la polisi
MBALI ya
jitihada mbalimbali zinazofanywa na makampuni ya kutengeneza pombe
kutoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya,
‘janki’ Geoffrey Mlelwa (26), mkazi wa Ipogolo mjini hapa, amejikuta
akiyakatisha maisha yake kwa kudaiwa kugida pombe kupindukia.Tukio
hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo kijana huyo alikuwa katika
Soko Kuu la Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake wakipiga ulabu kwa
staili ya kuchanganya (kuchoma sindano) ndipo Geoffrey alipopitiliza na
kusababisha apoteze uhai.
Wakizungunza
na mwanahabari wetu, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa kijana huyo enzi
za uhai wake alikuwa ni mtu wa kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi
na bangi ila siku hiyo alionekana mwenye ‘mihela’ hivyo kuachana na
kunywa pombe aliyoizoea na kuanza kunywa pombe ya kisasa kama grants,
viroba na kuchanganya na ulanzi ndani ya chupa moja.
“Mbali ya
‘kuchanganya madawa’, kijana huyo hakula chakula chochote tangu
alipoanza ‘kupiga vyombo’ na alipozidiwa, rafiki yake alimkokota na
kumpeleka chumbani kwao (geto) kabla ya asubuhi kuamka na kumkuta
amekufa,” alisema shuhuda mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Baba
mzazi wa kijana huyo (pichani) mzee Guriano Mlelwa alithibitisha
kutokea kwa kifo cha mwanaye na kuwa chanzo cha kifo hicho ni unywaji wa
pombe kupita kiasi.
Alisema
kuwa kwa kawaida kijana wake anamtambua kama ni mlevi wa pombe na
mtumiaji wa madawa ya kulevya na kuwa hata katika chumba chake
walimkutana na chupa ambayo ndani yake ilikuwa imechanganywa pombe
mbalimbali.
Alisema
anaamini kuwa mchanganyiko huo wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya
ndivyo vilisababisha kifo hicho hivyo kuwashauri vijana kuachana na
matumizi ya pombe kupita kiasi na madawa ya kulevya kwani wakiendelea
kilichomuua mwenzao ndicho kitakachowaua.
- GPL
No comments:
Post a Comment