Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) Dr Wilbrod Slaa akizungumza na wananchi wa Arusha katika viwanja vya Kilombero ikiwa ni mfululizo wa Mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi iliyoanza juzi katika maeneo tofauti ya nchi. Katika mkutano wa Arusha Dr Slaa aliambatana na viongozi wengine kutoka NCCR Mageuzi na Chama Cha Wananchi (CUF) iliyowakilishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bw Mustafa Mwanri.
Kutoka kushoto, Bw Elifuraha wa ArushaMambo Radio, Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa na Dr Slaa
Mwakilishi wa NCCR-Mageuzi
Mmoja wa wageni waalikwa akisaini kitabu cha mahudhurio
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika kutoka kwa vikosi vya vyama vyote vitatu. Pichani ni kijana wa Redbrigade ya Chadema Bw George katika suti maridadi.
Viongozi mchanganyiko wa vyama vyote vitatu. Katikati anaonekana Dr Slaa akiwa kulia kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Mh Philemon Ndesamburo ambaye amejitolea Helkopta yake pamoja na gharama za mafuta na rubani kuzunguka Kanda yote ya Kaskazini hadi Tarime Mkoani Mara.
Mustafa Mwanri wa CUF akizungumza na wananchi
Dr Slaa akikaribishwa Jukwaani
Mwakilishi kutoka Shura ya Maimamu akiwasilisha ujumbe wake.
Madiwani na na baadi ya viongozi
Mh Ndesamburo akifurahia jambo na mdau wa NCCR
No comments:
Post a Comment