Majeruhi bi Happiness Chacha (22)
akiwa amelazwa katika wodi namba 8 katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya
kuungua moto yeye na mme wake
-Picha zote na Valence Robert
Majeruhi Chacha Wambura (35)akiwa
amelazwa katika wodi namba 7 katika wilaya ya Geita baada ya kuungua moto
katika kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita.
Wanandoa wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani
Geita mkoani Geita Happiness Chacha(22)
na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuungua
moto katika kibanda chao cha bar.
Tukio hilo limetokea jana usiku saa
nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa ambapo kufuatia tukio hilo majeruhi
wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita mkoani Geita walipolazwa wodi
namba 7 na 8.
Robina Isack anayewauguza amesema kuwa usiku
huo wa saa 8 waliona moto unawaka bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa
vile hawatumii nishati hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa
wamewasha ndani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita
Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Valence Robert-Geita
No comments:
Post a Comment