Pages

Friday, May 9, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WA NIGERIA ALHAJ ALIKO DANGOTE JIJINI ABUJA

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika. Alhaj Dangote ni mwekezaji mashuhuri duniani na hivi sasa anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara.
 Mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki wakati Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana kwa mazungumzo na mfanyabishara huyo maarufu wa Nigeria jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono baada ya mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment