Pages

Wednesday, May 21, 2014

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.SHEIN ATEMBELEA BANDARI YA ZANZIBAR.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhamed Shein akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Affan Othman Maalim (alievaa suti bluu na kofia) baada ya kutembelea ghala lililokuwa likitumika  kuhifadhia pembejeo za kilimo alipotembelea bandari  hiyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhamed Shein akifuatana na viongozi wa Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano wakiingia lango kuu la Bandari ya Zanzibar iliyop Mlindi alipotembelea bandari hiyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Muhamed Shein akifuatana   na viongozi wa Shirika la Bandari  Zanzibar kuangalia utendaji wa kazi katika bandari hiyo ambayo hivi sasa meli kubwa ya makontena  zinafunga gati na kushusha  mizigo kwa wepesi.

 
 Gari la Scaner linalotumika kwa uchunguzi wa vitu vilivyomo ndani ya kontena liliopo katika Bandari ya Zanzibar likiwa limeegeshwa ndani ya bandari hiyo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhamed Shein akitembelea sehemu ya muda inayowekwa makontena katika  eneo la Hoteli ya Bwawani ambalo Serikali imelitenga kwa ajili ya kujenga maduka ya kisasa ya Wafanyabiashara..

No comments:

Post a Comment