Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Kusini wakiwa wamejitokeza katika usaili wa Kushiriki shindano la Tanzania Movie Talent katika Ukumbi wa Safari lounge uliopo Eneo la Maduka Makubwa, Mtwara Mjini wakiwa kwenye foleni tayari kwa shindano kuanza.
Kundi la Kwanza la Washiriki wa Kanda ya Kusini wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupewa semina elekezi juu ya maswala mbalimbali kuhusiana na filamu na maisha kwa ujumla wakati walipofika katika ukumbi wa safari lounge kwaajili ya kushiriki kwenye shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mjini Mtwara leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions wakiwabandika washiriki namba za ushiriki katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika katika Kanda ya Kusini, Mkoani Mtwara leo.
Washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakisubiri kuingia kwa majaji kwaajili ya kuanza kuonyesha Vipaji vyao vya kuigiza katika shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wakazi wa Mtwara waliojitokeza kushuhudia mchakato wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Mtwara
No comments:
Post a Comment