Jeshi
la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za kitamaduni
ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za
usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana
makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia
kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao
wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi
kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma
yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’
Kamanda
Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya
kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja ambapo pia
watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu vinavyofanyika nyakati za usiku
wakati wa ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la
polisi limetoa onyo kali kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment