Pages

Monday, May 26, 2014

TAZAMA PICHA ZA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TANESCO NA MKEWE WALIPOPANDISHWA KIZIMBANI KWA UBADHILIFU WA MIL 884,550,000



Askari kanzu akitanua njia wakati Mhando (mwenye shati jeupe) akipelekwa kizimbani.



Mhando (kushoto) na wenzake wakitoka mahakamani.



Waliounganishwa kwenye kesi hiyo nao wakishuka kizimbani chini ya ulinzi mkali.



Mke wa Mhando (kushoto) na mwenzake wakirudishwa mahabusu.
MKURUGENZI  wa zamani wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William Geofrey Mhando na mamsap wake, Eva Stephem Mhando, na maofisa wengine watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange, Sophia Athanas Misidai na Naftali Luhwano Kisinga,  leo wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000.
Katika kesi hiyo iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo alisema Mhando akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa  kumpa tenda mamsap wake ya kusambaza vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi milioni 884,550,000/ kwa shirika hilo kinyume na taratibu.
(PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/GPL)

No comments:

Post a Comment