Mtuhumiwa Mtonga Omari akitoka
mahakamani huku
mikono ikiwa kichwani akijutia
Unyama anayodaiwa kumfanya mtoto huyo wa
marehemu shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Mwasiti Said.
Watuhumiwa wa mtoto anayedaiwa
kufichwa kwenye boksi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Morogoro, kujibu mashtaka ya kula njama
na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.watuhumiwa hao waliofikisha mahakamani
hapo chini ya Ulinzi mkali ni Rashid Mvungi (47), washtakiwa wengine katika
kesi hiyo iliyovutia umati wa watu wa mji wa Morogoro ni mama mlezi wa Nasrah,
Mariamu Said (38) na mume wake Mtonga Omar (30).
Baba mzazi wa Nasra Bw Mvungi
aliyevaa shati la karoakiingia kwenye mahabusu ya mahakama ya mkoa akisubiri
kupelekwa gerezani baada ya kushinda kutimiza masharti ya dhamana,Wananchi
waliokuwepo mahakamani hapo walifurahia watuhumiwa hao kupelekwa magereza baada
ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Hatimaye wale
Washtakiwa hao walifikishwa katika
mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo, Jumatatu ya
wiki hii na kusomewa mashtaka hayo.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera
alidai kuwa washtakiwa walitenda makosa
hayo kati ya Desemba mwaka 2010 na Mei mwaka huu katika mtaa wa Azimio kata ya
Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi hicho,
washtakiwa wakiwa walezi wa mtoto Nasrah, walimfanyia ukatili wa mtelekeza na
kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa.
Wakili huyo wa Serikali, aliyataja
maradhi yaliyokumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi kuwa ni pamoja na
utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili wake.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
No comments:
Post a Comment