Pages

Thursday, May 22, 2014

TONI KROOS KUTUA MAN U KWA PAUNI MIL 20

Toni Kroos.
MANCHESTER UNITED imekubali kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos kwa pauni milioni 20 sawa na bilioni 55.8 za Tanzania.
Arjen Robben.
Mchakato wa kumnasa kiungo huyo mwenye miaka 24 ulianzishwa na kocha aliyetimuliwa baada ya kuboronga, David Moyes na sasa umepewa baraka na kocha mpya Louis van Gaal.
Timu hiyo kwa sasa inajipanga kumnasa mshambulaji hatari wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Uholanzi, Arjen Robben.
Mashetani hao Wekundu tayari wamekubaliana kiasi cha pauni milioni 27 na beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw.
Mbali na Robben, Gaal pia anamuwinda beki wa kati wa Borussia Dortmund, Mats Hummels.

No comments:

Post a Comment