Pages

Sunday, May 25, 2014

UCHAFU ULIOKITHILI KATIKA SOKO LA MJENGO WAZUA HOFU YA GONJWA LA DENGUE MKOANI DODOMA

 Takataka zikiwa zimejazana katika soko kuu la majengo Manispaa ya Dodoma katika eneo la yadi ambapo bidhaa za sokoni hushushiwa, hali inayotishia magonjwa ya milipuko kwa wafanyabiashara.
 Maji machafu yanayotililika toka katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma yakiwa yametuama kwenye mtaro unapita katika ya soko kuu la majengo hali iliyozua hofu kubwa ya kulipuka kwa Gonjwa Hatari la Dengue kwa wafanya boashara sokoni hapo.


Mmoja wa wachanjaji wa kuku katika eneo la soko la majengo mjini Dodoma akinyonyoa manyoya ya kiuku katika eneo lisilo rasmi ambalo pia ni hatari kwa afya zao na za wanunuzi kutokana na uchafu kuzagaa hovyo.

 Na John Banda, Dodoma
WAFANYABIASHARA wa soko kuu la Mjengo Manispaa ya Dodoma wamekumbwa na wasisiwasi  wa kukumbwa na ugonjwa hatari wa Dengue , kutokana na mlundikano mkubwa wa uchafu na maji kutuama katika mfeleji unaopitisha maji machafu katikati ya soko hilo.



Wasiwasi huo uliotolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo unaonyesha kushtushwa na taarifa za kulipotiwa kwa wagonjwa wawili kuugua ugonjwa huo mkoani hapa. Ramadhani Muzazis (Mzee wa Langolango) alisema wafaanyabiashara sokoni hapo wanawasiwasi mkubwa wa kukumbwa na gonjwa hilo tishio kwa sasa nchini kutokana na uchafumwingi kulundikana kwa muda mrefu kwenye
Dampo lilipo karibu na meza zao za biashara. Langolango alisema   kutoondolewa kwa uchafu huo na maji machafu yanatoka katika hospital ya Rufaa ya Dodoma [General]  na majani
marefu yaliyomea bila kufyekwa kwa  muda mrefu ni hatari inayowakumba kutokana na mazalia ya Mbu na si ajabu Dengue akawepo na kisha kuusambaza ugonjwa huo.
Alisema wafanyabiashara wamekuwa wakilipa kodi za majengo na ushuru mbalimbali sokoni hapo kwa manispaa lakini hadi ugonjwa huu unapiga hodi na kuingia mkoani hapo hakuna lolote lilifanywa na manispaa ili kudhibiti uchafu na maji hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Afya katika soko hilo Roda Matonya alisema wafanyabiashara tayali wamejipanga kufanya usafi wenyewe kutokana na kuchwa na watendaji wa manispaa ambao mara nyingi wamekuwa wakivutana nao sana kuhusu majukumu yao ya kuhakikisha soko hilo ni
safi.
Roda aliongeza kuwa kwa sasa wana uzoefu  kuwa manispaa wakifika na kufanya usafi sokoni hapo basi wanampango wa kupandisha kodi au ushuru, hali ambayo inawafanya kuchukua hatua wenyewe ya kufanya usafi na kuua mazalia ya mbu ili kuepukana na Dengue.
 ‘’Pamoja na kulipia pango na ushuru lakini tumekuwa tukivutana sana na manispaa ambao kwa kweli wameshindwa kuliondoa hilo Dampo linalokusanya uchafu mwingi karibu kabisa na wafanyabiashara, unadhani hili hiyo kuna mfanyabiashara ataacha kugongwa na huyo mbu aneambukiza Dengue?’’, alihoji Roda.

No comments:

Post a Comment