Wabunge wanaowakilisha chama kipya cha kupigania haki za kiuchumi za Waafrika Kusini
(Economic Freedom Fighters EFF) leo walizua kihoja baada kuingia bungeni wakiwa wamevalia kama wafanyikazi wajakazi na wachimba migodi .
Wabunge wanawake walivalia sare za mayaya na
wahudumu wa nyumbani huku wabunge wanaume wakivalia magwanda kama yale
yanayotumika migodini na wafanyikazi wanakandarasi.(Economic Freedom Fighters EFF) leo walizua kihoja baada kuingia bungeni wakiwa wamevalia kama wafanyikazi wajakazi na wachimba migodi .
EFF inayoongozwa na aliyekuwa kiongozi wa kitengo cha vijana katika ANC Julius Malema ilishinda viti katika maeneo bunge 25 katika bunge hilo lenye uwakilishi bunge 400 katika uchaguzi uliofanywa majuzi.
Malema aliyeunda chama hicho baada ya kutimuliwa kutoka kwenye ANC mwaka wa 2012
Malema aliibua hisia miongoni mwa mamilioni ya wapiga kura Waafrika weusi aliposema kuwa atapeleka miswada bungeni kwa lengo la kutaifisha mashamba ya wazungu wachache ilikupunguza mzigo wa umasikini.
Mwandishi wa BBC aliyeko Cape Town Afrika Kusini Pumza Fihlani,anasema mavazi hayo ya wabunge wa EFF yalikuwa ya kipekee kwani wenzao walikuwa wamevalia mavazi ya kifahari na suti zinazotengenezewa ughaibuni.
Mbunge wa EFF Floyd Shivambu
" hatimaye wanyonge wamepata waakilishi katika bunge."
Hata hivyo mwandishi wetu anasema kuwa idadi yao ndogo ambayo ni takriban asilimia 6% ya wabunge 400 haitawaruhusu kupitisha miswaada waliowaahidi wapiga kura wao.
Chama tawala cha ANC kilipata asilimia 62% ya kura zote huku chama cha Democratic Alliance (DA) kikizoa asilimia 22% ya kura zote .
Kikao hicho cha bunge kilikuwa mahsusi kuwaapisha wabunge wapya hata hivyo rais Jacob Zuma anatarajiwa kuapishwa siku ya jumamosi.
No comments:
Post a Comment