Pages

Friday, May 2, 2014

Wadau wa elimu mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wiki ya elimu itakayo fanyika kitaifa mkoani Dodoma.

 


Wadau wa elimu mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wiki ya elimu itakayo  fanyika kitaifa  mkoani  Dodoma.
Akizungumza katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi  Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma  Dr Rehema nchimbi amesema  mkoa wa Dodoma ndio mwenyeji wa sherehe hiyo kutokana na kwamba itazinduliwa Kitaifa Mkoani hapa katika viwanja vya jamhuri.
Aidha Dr Nchimbi  amezitaka taasisi zote za elimu kuweka mabanda katika viwanja vya jamuhuri ili kuonyesha utendaji kazi wa taasisi hizo.
Pia amekitaka chama cha walimu CWT kuweka banda katika viwanja hivyo  ili watu wakitambue chama hicho na kuwataka walimu kuwa na mshikamano ili kufanikisha wiki ya elimu kikamilifu.
Maadhimisho ya wiki ya Elimu yanatarajiwa kuanza  tarehe 3Mei mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment