Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 2, 2014

Wafanyakazi Ruvuma watakiwa kutimiza wajibu na kisha kudai haki

 Wakati kati ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo  Abdula Lutavi
 -----------------
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
SERIKALI ya mkoa wa Ruvuma imeendelea kuwasihi wafanyakazi wa sekta zote nchini wasijenge zaidi utamaduni wa kudai haki bila kutimiza wajibuwao kwanza kwa sababu kauli mbiu za vyama vingi vya wqafanyakazi kikiwemo chama cha walimu nchini ambacho kauli mbiu yake  ni wajibu na haki.

Kauili hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdula Lutavi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo amesema baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wamekuwa hawatimizi wajibu wao ipasavyo lakini ndiyo wanakuwa msitari wa mbele kulaumu na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wao kwanza kwa mwajiri.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA Songea wakipita mbele ya jukwaa kuu huku wakionyesha mavazi wanayoshona chuoni hapo ikiwemo mavazi la maharusi na ya ulimbwende.
-----------------------------------
Amesema sekta ya elimu ndiyo yenye watumishi wengi ambao wapo katika kila kijiji nchini na ndiyo wataalamu wanaotumiwa na wananchi wa maeneo hayo lakini baadhi yao wamekuwa ni watoro na wazembe katika maeneo yao ya kazi na kutotimiza wajibu wao kwa makusudi na kwa visingizio mbali mbali na wakiendelea kulindwa na walimu wakuu pamoja na wakuu wa idara za kielimu hali ambayo inazidi kudumaza kiwango cha elimu mkoani Ruvuma na kuufanya mkoa kuendelea kutofanya vizuri katika sekta hiyo muhimu.
Mtangazaji wa TBC mkoani Ruvuma Noela Njawa akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
---------------------
Aidha amesema walimu watoro na wazembe ndiyo wanakuwa wa kwanza kulaumu na kulalamikia masilahi duni na kuhamasisha migomo ambayo imekuwa ikiwaathiri wanafunzi pasipo sababu huku serikali ikionenesha nia kuongeza na kuboresha maslahi yao ikiwa ni pqamoja na kulipa malimbikizo mbali mbali wanayoidai serikali ambayo taratibu za malipo zinaendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika.

Nao wafanyakazi wa sekta mbali mbali mkoani Ruvuma katika risala yao kwa mgeni rasmi wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo cha taifa kuadhimidsha miaka hamsini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku taifa likiwa salama kutokana na dhana iliyojengeka ya kuzingatia  utawala bora katika kila Nyanja lakini bado kumeendelea kuwepo kwa matatizo ya madeni ya watumishi,mishahara duni na waajiri kutokujali sheria za kazi vitu ambavyo vimekuwa vikiendelea kugonga vichwa vya wafanyakazi walio wengi na kupunguza morali ya kazi.
Mfanyakazi wa Idara ya wakala wa majengo Mkoa wa Ruvuma Wizara ya Ujenzi Bw. Charles Buhili akipokea zawadi ya mfanyakazi bora.
----------------------
Wamesema imekuwa ni kawaida kwa watumishi wa umma kupewa ahadi kila mara za kupunguziwa matatizoi yao katika maeneo yao ya kazi yakiwemon madeni ya muda mrefu ya watumishi hao lakini utekelezaji wa ahadi hizo umekuwa ni wa kusuasua pamoja hali ya haslisi ya kiuchumi wa taifa ikijulikana hali imekuwa ikiwavunja moyo watumishi walio wengi wa umma kutimiza wajibu wao.
Mlinzi wa CCM mkoa wa Ruvuma Bw. Mika Nchimbi akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
------------------------
Aidha wafanyakazi katika risala hiyo wametoa maoni kuwa utekelezaji wa ahadi hizo ungekuwa unapewa uzito kama vile zinavyotolewa kwa msisitizo na viongozi mbali mbali wa serikali na waajiri kikiwmo kilio cha muda mrefu cha kodi kubwa kwa wafanyakazi walioko kwenye mfumo rasimi ambao wamekuwa wakikatwa kodi hiyo moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao ambayo haikidhi mahitaji ikilinganishwa na gharama za maisha ya kila siku.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment