Aidha, katika matukio hayo, mali mbalimbali kama vile simu, kompyuta mpakato na nguo, viliibwa.
Kutokana
na matukio hayo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeagiza uongozi wa
vyuo vya elimu ya juu nchini, kutumia askari polisi wasaidizi au
kuanzisha vituo vya askari kwenye maeneo ya makazi ya wanafunzi na
vyuo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema
hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kaskazini,
Charles Mwijage (CCM) aliyetaka kufahamu mpango wa serikali kuhakikisha
maeneo yote ya vyuo vikuu, yanapewa ulinzi wa uhakika baada ya
kujitokeza hali ya uvamizi katika makazi na maeneo ya vyuo vikuu.
Pia, mbunge huyo alitaka kufahamu idadi ya wanafunzi walioshambuliwa na mali zilizoharibiwa kutoka kwa wanafunzi hao.
Naibu
waziri alisema ulinzi na usalama wa raia, wakiwemo wanafunzi wa shule
na vyuo vikuu ni muhimu kwa mustakabali wa elimu ya vijana nchini.
Alisema ni jukumu la wote, kama sehemu ya wajibu wa kikatiba na kijamii.
Alisema
jeshi la polisi ndicho chombo chenye dhamana ya kusimamia wajibu huo,
litaendelea kuchukua hatua za kupambana na vitendo vya uvamizi na
uharibifu mwingine, unaotokea katika vyuo hivyo nchini hususan vya elimu
ya juu.
Alisema wanaendelea kushirikiana na mamlaka, hususan uongozi
wa vyuo, halmashauri, miji na serikali za mitaa kuweka miundombinu ya
ulinzi shirikishi utakaosaidia kukabili matukio ya uhalifu.
“Aidha,
napenda kuwaasa wanafunzi wa vyuo kutojihusisha na shughuli na
mazingira hatarishi kwa usalama wao na mali zao,” alisema.
Katika
swali lake la nyongeza, Mwijage alitaka kufahamu ni mikakati gani ya
serikali kuweka vifaa vya usalama katika shule ili kukabiliana na
uvamizi katika vyuo hivyo.
Akijibu swali hilo, Silima alisema ulinzi
hasa wakati huu wa matishio ya vitendo vya kigaidi ni muhimu katika vyuo
vya elimu na sehemu nyingine zenye mikusanyiko katika maeneo muhimu,
kama vile hoteli.
Aidha, alisema ni vyema kuweka utaratibu wa kupekua kila anayeingia kuepuka kuingia mtu atakayesababisha madhara.
No comments:
Post a Comment