WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda (pichani) amesema Serikali itaendelea kusimamia msimamo wake
wa kutokuwa na dini wala nchi kutokuwa na dini lakini itaendelea kuruhusu watu
wawe na dini zao.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka wakfu
Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko nje ya nchi kikazi, alisema: “Leo
tukiruhusu Serikali iwe na dini na tayari katika dini zote kuna makundi madogo
madogo, je wale wa upande mwingine utawaacha wapi?”.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa
dini nao pia waangalie wasitumbikie kwenye mtego wa siasa na kuruhusu kanisa
zima liwe la chama fulani kwani miongoni mwa waumini wao wapo pia wapenzi wa
vyama vingine.
“Kama mtu binafsi, kiongozi wa dini anaweza
kuwa mpenzi wa chama lakini kama Kanisa tusiruhu hali hiyo,” alionya.
Aliwaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea
Taifa na hasa waombee amani ya Taifa hili. “Ninawasishi viongozi wa dini
msichoke kuombea amani ya Taifa hili kwani amani ikipotea kama nchi hatuna
mahali pa kukimbilia."
No comments:
Post a Comment