Waziri wa michezo nchini Afrika
Kusini, Fikile Mbalula amekemewa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya
kwa matamshi yake kuhusu wanariadha wa Kenya.
Waziri huyo inaarifiwa alitoa matamshi yake
katika mkutano na wandishi wa habari mjini Johannesburg alipokuwa
anazungumzia swala la utangamano katika jamii."huwezi kuleta mageuzi katika michezo bila malengo,'' alinukulwia na jarida la Mail and Guradian akijibu swali hilo kuhusu swala tete la ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
"lakini Afrika Kusini haiwezi kuwa kama Kenya na kutuma wanariadha wake katika michezo ya Olimpiki wakazame kwenye vidimbwi vya kuogelea,'' aliongeza waziri huyo.
Kulingana na jarida la Mail & Guardian, matamshi ya waziri huyo yaliwashangaza wengi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo baadhi hata wakigeuka kwa aibu.
Ikiwa matamshi ya waziri huyo yangetafsiriwa kwa maana ya juu juu, basi sio kweli. Hakuna mkenya yeyote aliyewahi kuzama katika kidimbwi katika michezo ya Olimpiki.
Wakenya wajitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumjibu waziri huyo baadhi wakisema kuwa hayo yalikuwa matusi kwa wakenya.
Baadhi walihisi kama waziri huyo alikuwa anadharau wanariadha wakenya ambao wameiletea nchi yao sifa kedekede katika riadha kimataifa.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment