WATU wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika
matukio tofauti, likiwemo la mmoja aliyekutwa amekufa akiwa katika basi la
Kampuni ya Kilenga akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro, Moita Koka, alisema kuwa mtu huyo ametambuliwa kwa jina la
Sayuni Joel (53), mfanyabiashara, mkazi wa Mwembe, wilayani Same, Kilimanjaro.
Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Kamanda Koka alisema
Joel alipanda basi hilo T 398 BAT na kwamba kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa
akisumbuliwa na tumbo na alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu.Alisema
Joel aligundulika kuwa amepoteza maisha baada ya gari hilo kuingia katika
stendi kuu ya mabasi Moshi.
Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC
huku uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho ukiendelea.Katika tukio jingine, mkazi
wa Kijiji cha Kilema – Kiyou, Kata ya Kilema, wilayani Moshi, Martin Michael
(45), amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema lilitokea juzi, saa 8
mchana na kudai kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na hali yake
kiafya ambayo imemfanya kutumia dawa kila mara na kwamba kabla ya tukio hilo
aliwahi kusikika akilalamikia hali hiyo.
Na Dixon Busagaga, moshi
No comments:
Post a Comment