Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza tukio ambapo
mwanamume mmoja anaripotiwa kumuaa mwanamue mwingine aliyekuwa na uhusiano na
kimapenzi na mwanamuke anayeaminika kuwa mpenzi wake wa zamani.
Alimuua ka kumkatakata vipande na kisha kuula Moyo wake.
Majirani eneo la Malunga lililo katika mji wa Gugulethu nje
ya mji wa Capetown, wanasema kuwa walikumbana na
mwanamume aliyeshuhudia mauaji
hayo siku ya Jumanne.Walioshuhudia wanasema kuwa wakati walipofika katika mtaa
wa kifaharai ambako mshukiwa alikuwa anaishi walimsikia akisema kuwa "ni
yeye mfalme" akisema kuwa bado anampenda mpenzi wake wa zamani.
Kwa sasa anazuiliwa na polisi
Polisi mmoja aliiambia BBC kuwa wakati walipowasili eneo la
tukio walimpata mshukiwa akila moyo wa binadamu akitumia uma na kisu.Walifahamishwa
kuwa mwathiriwa alidungwa kisu upande wake wa kushoto kifuani na kwenye shingo
lake na katika sehemu ya uso alikuwa na alama ya kuumwa.Marehemu anayeaminika
kuwa Bwana Mbuyiselo Manona,alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyekuwa
mpenzi wa mshukiwa kwa miaka minne.
Hapakuwa na dalili zozote za mwanamke huyo nyumbani kwake
Jumatano lakini gari lake lilikuwa limeegeshwa nyumbani kwake.Inaripotiwa si
mara ya kwanza mwanamke huyo ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka 50
kuhusishwa na visa vinavyohusiana na mapenzi. Mumewe aliuawa na mtu anayekisiwa
kuwa mpenziwe mwaka 1996.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment