BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 maeuawa katika
mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma
ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundo hilo yapata siku 50 zilizopita.Wakaazi
wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema
kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza
watu waje katika uwanja wa kanisa.Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa
wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao
kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.Mbunge
wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi
wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.
Jeshi lakanusha madai
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha madai katika
vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imewapata na hatia
baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia wapiganaji wa Boko Haram.Msemaji
kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi
waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.Jeshi limesema kuwa taarifa hizo
ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
nyumba zimechomwa Borno
Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa
maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio
yaliyochacha.Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na
kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.Suala la wasichana
waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria
ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa
haraka.Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na
tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani
yanaweza kufanywa.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment