Hapa mangumi tu: Guillermo Ochoa akiokoa mpira wa hatari
uliopigwa na Paulinho.
ULIKUWA usiku muhimu kwa Brazil katika mechi ya pili ya
kundi A ya kombe la dunia mwaka 2014, lakini safari hii imedhihirisha kuwa si
lazima wapate kila wanachokihitaji katika michuano hii.
Mashabiki wa Brazil kutoka kila kona ya nchi hiyo walifurika
uwanjani kuwaona mashujaa wao na timu hiyo ya Luiz Felipe Scolari ilijitahidi
kwa nguvu zote kutafuta magoli yatakayowafurahisha na hatimaye kuambulia
ushindi wa pili, lakini walikumbana na kisiki cha Mpingo, Mexico.
Isingekuwa mlinda mlango wa Mexico, Guillermo Ochoa, Brazil
wangebaki na furaha. Aliiokoa timu yake katika hatari mbili Au tatu katika
kipindi cha kwanza, lakini hatari moja ameokoa katika dakika za mwisho na
kulazimisha mechi kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Neymar akiwa ameanguka chini baada ya kufanyia rafu na
Wamexico.
Ngado kwa ngado!Neymar akijaribu kuwatoka mabeki watatu wa
Mexico usiku huu uliokuwa mbaya kwa Wabrazil.
Neymar akipiga mpira wa adhabu, lakini uliokolewa na mlinda
mlango wa Mexico (chini).
Neymar alijikuta yupo ndani ya nyavu lakini mpira ulikuwa nje
No comments:
Post a Comment