Pages

Thursday, June 19, 2014

CAMEROON YATPWA NJE KOMBE LA DUNIA,TAZAMA PICHA WACHEZAJI WAO WAKIPIGANA UWANJANI

Kitu cha pili kambani:  Ivan Perisic (wa pili kulia)akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili.
KITENDO cha Alex Song kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Croatia, Mario Mandzukic na kuoneshwa kadi nyekundu rasmi kimeua matumaini ya Cameroon kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia katika kundi A mjini mjini Manaus.Song alishikwa na hasira dakika ya 40 na kufanya kitendo cha kinyama kwa Mandzukic wakati huo Cameroon ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
Baada ya Hispania kutupwa nje ya michuano, Cameroon imekuwa nchi ya kwanza kwa Afrika kufangasha virago katika fainali za kombe la dunia mwaka huu kutokana na kipigo kikubwa cha mabao 4-0 dhidi ya Croatia.
 Kufuatia kadi nyekundu ya Song, mambo yalikwenda kombo zaidi na kushuhudia Cameroon wakimalizia usiku vibaya baada ya kufungwa mabao matatu kipindi cha pili na ndoto za kufuzu kuzimwa kabisa.
Hata hivyo kituko kikubwa ni beki wa Tottenham Benoit Assou-Ekotto  kuamua kupigana na mwenzake Benjamin Moukandjo katika  hatua za mwisho za mchezo huo.

Assou-Ekotto na Moukandjo wakitunishiana misuli baada ya kutofautiana

 Chukua kichwaaa hichooo dogooooo usilete maneno tena sawaaaa
 Ahhhhh wewe unampiga nani?Moukandjo akimkaba Assou-Ekotto baada ya kupigwa
 unazingua sanaa weweeeee akissema Moukandjo
 Samuel etoo akimtulizaaaa Assou-Ekotto baada ya kutaka kurudi kupigana tena
 Etooo niachieee yule dogo mbishii nikamfunze adabuuu

No comments:

Post a Comment