‘Die hard fans’ wanaweza kufanya lolote kuhakikisha wanampa
ushindi msanii wao katika shindano lolote linalohiotaji ushiriki wao hasa wa
kupiga kura au maoni, kama kinachofanywa hivi sasa na mashabiki wa Diamond
Platnumz katika tuzo za BET.
BET wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za
mitandao ya kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea ushawishi wa
kupewa ushindi wasanii wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya Diamond imeendelea
kupata likes na comments nyingi katika Facebook ya BET, mpaka sasa ina likes
2649 na comments 5471 huku Davido akiwa na likes 1465 na comments 619 tu.
Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa
jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win
#BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,
Hadi sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya
Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina
likes 518 na comments241 tu
Cha kushangaza mashabiki wa Diamond wameamua kutoka nje ya
kile kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment jina la Diamond katika picha
hiyo ya Davido.
No comments:
Post a Comment