Ijumaa iliyopita, Wababa ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya
kuimba ya Bongo Star Search aliwalalamikia maswaiba Nay wa Mitego na
Diamond Platinumz kwa wizi wa kazi zake kwa wakati tofauti na njia
tofuati alipoongea katika Friday Night Live ya East Africa Radio.
Wababa
alidai Diamond amemuibia wimbo wake wa Kitorondo ambao aliufanya na
Dogo Aslay miaka karibu minne iliyopita na akafanya hadi video na iko
kwenye mtandaoni.
Lakini pia alimtuhumu Nay wa Mitego kwa kupanga njama za kutaka kumuibia wimbo wake aliomshirikisha ndani ya Mazoo records ambapo Nay wa Mitego anadaiwa kumtafuta Mazoo kimya kimya na kutaka kumlipa mkwanja ili amkabithi wimbo huo kinyamela na kumtosa Wababa.
The True Boy himself amefunguka kuhusu Tuhuma za Wababa:
“Sijui niongee nini kuhusu hii issue…mimi nimeisikia. Lakini mimi
napenda beat nzuri, mimi sijataka ile beat. Lakini kilichofanyika ni
kwamba producer ametaka kunipa mdundo wa design ile lakini sielewi ni
kwa nini tena maneno yamekuja kwamba mimi nimetaka kuilipia ile beat.
No, mimi nilisema
napenda ule mdundo wa design ile kwa gharama yeyote naweza nikaulipia lakini sio kama nimetaka mdundo wa dogo..no.
napenda ule mdundo wa design ile kwa gharama yeyote naweza nikaulipia lakini sio kama nimetaka mdundo wa dogo..no.
“Ngoma ya dogo nzuri, mimi mwenyewe nimependa the way nilivyoimba
lakini sio kama nitake ngoma yake au beat yake hapana ntakuwa nakosea,
nitakuwa nakosea sana. Lakini mimi nilichoongea ni tofauti na hicho
labda wale wameninukuu vibaya. Mwisho wa siku naweza kusema mimi
siwezi…kwanza muziki wangu watu wanaujua uko tofauti sana. Hiyo ngoma
yenyewe ukiisikia iko tofauti sana, na mimi nimetaka changes kwenye
muziki wangu.. nilimwambia producer nataka beat ya design hii ambayo
inaweza kuwa kali zaidi ya hii na mimi nikailipia hela yoyote
unayoitaka. Kwa hiyo mwisho wa siku sijui nini kiliendelea hapo
katikati.
“Si kweli…ni nyimbo nzuri kweli mimi niliipenda niliisifia na
ndio maana nilikuwa na nguvu ya kuweza kuifanya naweza kusema kwa
asilimia mia moja. Mimi sijafanya featuring tangu mwaka jana. Kwa mwaka
huu nilifanya featuring mbili tu, nilifanya ya kwanza ya Kala Jeremiah
na hii ni ya pili tena baada ya kutumiwa demo nikaoni ni nzuri sana.
Niliifanya kwa nguvu kwa sababu niliona ni nyimbo nzuri ambayo hata mimi
mwenyewe watu wanaweza kuendelea kusema ‘okay mwana amefanya collabo
nzuri’. Siwezi kuchukua nyimbo yake yeye, nyimbo yake yeye.
“Mimi anitafute, siku mbili tatu hizi nilikuwa busy na mambo
yangu. Nilikuwa namalizia nyumbani kwangu huku na kule vitu vingi shows
na vitu vingine. Anitafute tutaongea. Mimi naweza kusema hivi ni mdogo
wangu, hakuna ambacho kitaharibika lakini sidhani kama itaweza kufikia
hatua tukagombana mimi na yeye. Labda yeye alininukuu vibaya.”
Credit: Timesfm.co.tz
No comments:
Post a Comment