Na Insp. Deodatus Kazinja,PHQ
Aliyewahi kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la
Magereza Mzee Josephat Mwingira aliyefariki tarehe 09 Juni, 2014 na kuzikwa
tarehe 12 Juni,2014 katika Makaburi ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar
es salaam kwa heshima zote za kijeshi.Marehemu Mwingira aliajiriwa katika Jeshi
la Magereza tarehe 11 January 1956 ambapo alianzia kazi katika Gereza Kuu
Butimba la Jijini Mwanza na maeneo mengine mengi nchini hadi alipo staafu kwa
mujibu wa sheria tarehe 01 Julai, 1990 akiwa amelitumikia Jeshi la Magereza kwa
miaka 33.Hayati Mwingira mbali na kuwa kiongozi katika Jeshi la Magereza lakini
pia alikuwa kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alishika nyadhifa
kadhaa enzi za siasa majeshi.
Marehemu Josephat Mwingira
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiingiza
mwili wa Marehemu na kuuingiza nyumbani kwake baada ya kutoka “mortuary”.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Mmeta Manyara (wa kwanza kushoto) akitoa heshma zake kwa marehemu
Baadhi ya wastaafu wa Jeshi la Magereza wakitoa salamu za
mwisho kwa marehemu Mwingira (wa kwanza mbele) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa
Magereza Saimon Mwanguku, wa pili ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Alhaji
Jumanne Mangara. Wawili hao walifanya kazi kwa karibu sana na Marehemu Mwingira
enzi za uhai wake.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioko
kazini na wastaafu kwa pamoja wakijumuika na wananchi wa kijiji cha Kilongawima
Kata ya Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na wanafamilia katika
safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira
Askari wa vyeo mbalimbali wakijumuika na wananchi wa kijiji
cha Kilongawima Kata ya Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na
wanafamilia katika safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira.
Mwenyekiti wa CUF Taifa na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba
Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kuli waliokaa kwenye viti) alikuwa miongoni mwa
wananchi wa eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi Jijini Dar es salaam katika
kuifariji familia katika msiba huo mzito.
Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi (mwenye nguo
nyeusi) alikuwa miongoni mwa wananchi wa eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi
Jijini Dar es salaam katika kuifariji familia katika msiba huo mzito. Marehemu
Mwingira ni mzaliwa kijiji cha Mbaha Kata ya Lituhi Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Mwingira wakiweka
mashada ya maua.
Ibada ya mwisho makaburini iliyoongozwa na Padre Paul
Chiwangu kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania pamoja na Paroko wa
Parokia ya Mtongani Padri Paul Malewa.
Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza
walioshirikia katika kuandaa na kufanikisha paredi la mazishi ya Marehemu
Mwingira.
Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Mwingira wakiweka
mashada ya maua.
Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, Makao Makuu ya
Magereza
No comments:
Post a Comment