Pages

Saturday, June 21, 2014

KOLO,YAYA TOURE WAPATWA NA MSIBA WA MDOGO WAO


Ni msiba mzito umeikumba Kambi ya timu ya Taifa ya Ivory Coast baada ya wachezaj iwake muhimu Kolo na Yaya Toure kupata msiba mkubwa wa kufiwa na mdogo wao wa damu aitwae Ibrahim Toure, aliyefariki mapema leo kwa Ugonjwa wa Kansa. Na hivi sasa wachezaji hao wanataraji kurudi kwa Abdijan kutoka walipo na timu hiyo nchini Brazil kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa ajili ya taratibu za mazishi ya mdogo huyo aliyefariki jijini Manchester alipokuwa anakaa kwa kaka yake Yaya ambaye ni kiungo nyota wa Mabingwa wa soka England Man City. Ibrahim ambaye alikuwa pia ni mwanasoka mahiri katika nafasi ya ushambuliaji alishawahi kuzichezea club za El Magassah ya Egypt na El Safa ya Lebanon alikuwa ni mmoja kati ya mastaff wakubwa ndania ya timu ya Man City kiasi cha kuweza kusafiri na timu kwenye mechi zake kwa umaarufu wa kaka yake Yaya.

No comments:

Post a Comment