Ndugu zangu, hali ya ajira nchini ni mbaya sana. Idara ya
Uhamiaji imetangaza nafasi za kazi 70 kwa wahitimu wenye shahada moja na
kuendelea. Matokeo yake, baada ya mchujo wa majina zaidi ya 20,000; uongozi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, umepitisha majina ya waombaji 10,800 ili
washindanie hizo nafasi 70.
Kwa mara ya kwanza katika hostoria ya Tanzania, usaili kwa
ajili ya kujaza nafasi hizo 70 utafanywa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
mnamo Juni 13, mwaka huu saa 1:30 asubuhi! Hii haijawahi kutokea.
Tatizo la ajira kweli ni janga la kitaifa kwa sasa. Hawa
vijana wote wanaohitimu bila kuwa na kazi za kufanya, ni hatari sana kwa
usalama wa nchi kwa sababu sidhani kama watakubali kuendelea kusota mitaani
ilhali wakiwa hawana ajira. Tujadili jambo hili ili kuona namna nzuri ya kukabiliana
nalo.
No comments:
Post a Comment