Bosnia-Herzegovina imethibitisha kikosi chake kwa ajili ya
kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Ervin Zukanovic ameondolewa katika kikosi hicho baada ya
kushindwa kusafiri na timu kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kambi kutokana
na kukosa Visa.
Beki huyo wa Gent alikaririwa akililalamikia shirikisho la
Bosnia kwa tukio hilo, lakini viongozi walithibitisha kuwa mchezaji huyo
hatakiwi tena Brazil.
Kocha wa Bosnia, Safet Susic awali alitaja kikosi cha
wachezaji 24, hivyo kukosekana kwa Zukanovic kunamaanisha wachezaji wengine
wote waliocgaguliwa awali wataenda Brazil.
Bosnia watacheza na Mexico katika mechi ya mwisho ya
kujipima ubavu kesho jumatano, kabla ya kuvaana na Argentina, Nigeria na Iran
kwenye Kundi F kombe la dunia.
Kikosi Kizima hiki hapa:
Walinda Mlango: Asmir Avdukic (Borac Banja Luka), Asmir
Begovic (Stoke City), Jasmin Fezjic (Aalen).
Mabeki: Muhamed Besic (Ferencvaros), Ermin Bicakcic
(Eintracht Braunschweig), Sead Kolasinac (Schalke), Emir Spahic (Bayer
Leverkusen), Toni Sunjic (Zorya), Ognjen Vranjes (Elazigspor).
Viungo: Anel Hadzic (Sturm Graz), Izet Hajrovic
(Galatasaray), Senijad Ibricic (Erciyespor), Senad Lulic (Lazio), Haris
Medunjanin (Gaziantepspor), Zvjezdan Misimovic (Guizhou Renhe), Mensur Mujdza
(Freiburg), Miralem Pjanic (Roma), Sejad Salihovic (Hoffenheim), Tino Susic
(Hajduk Split), Edin Visca (Istanbul BB), Avdija Vrsajevic (Hajduk Split).
Washambuliaji: Edin Dzeko (Manchester City), Vedad Ibisevic
(Stuttgart).
No comments:
Post a Comment