Pages

Friday, June 20, 2014

MARA BAADA YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUMALIZIKA KANDA YA PWANI, WATANZANIA SASA KUANZA KUWAPIGIA KURA WASHINDI‏

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions katika Mradi wa Kusaka vipaji vya Kuigiza Nchini TMT (Tanzania Movie Talents) wakishangilia kwa kufungua Mvinyo usio na kilevi mara baada ya kumaliza zoezi la Kuzunguka Katika Kanda Sita nchini kwa kusaka Vipaji vya kuigiza ambapo zoezi hilo lilimalizika katika Kanda ya Pwani, Mkoani Dar Es Salaam ambapo washindi watano kutoka kanda ya Pwani walipatikana na Kupewa zawadi zao za Shilingi laki Tano Kila Mmoja na Kushiriki katika fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Mmoja wa Majaji katika Shindano la TMT Yvonne Cherry au Monalisa akifurahia kufungua Mvinyo huku wafanyakazi wa Proin wakifurahia pia kwa kukinga mvinyo huo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Pwani ambapo ndio imefunga zoezi hilo lililoanzia Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies,Bw Johnson Lukaza akiongea na wafanyakazi wa Proin Promotions limited mara baada ya kumaliza vizuri kwa kazi za kutafuta vipaji katika Kanda Sita za Tanzania.Pamoja na kuongea na wafanyakazi hao aliweza kutoa neno la shukrani kwa kila mmoja kwa kutimiza wajibu wake na hatimaye kufanikisha zoezi hilo la hatua ya kwanza kumalizika vyema.

 
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar es Salaam.
Safari ya Kutafuta vipaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambapo timu nzima ya TMT ilikuwa katika kanda hiyo kwaajili ya kusaka vipaji kupitia shindano hilo kubwa na la kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati. Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano ambalo lilizunguka kanda zote sita za Tanzania na hatimaye kilele chake kilimalizika mnamo tarehe 18 Juni 2014 katika Ukumbi  wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam katika Ukanda wa Pwani na kupelekea washindi watano kupatikana na kukabidhiwa Shilingi laki tano kila Mmoja.
Mara baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza ya kutafuta washindi kutoka kanda zote sita sasa ni wakati wa washindi wa kanda hizo kuja jijini Dar es Salaam na Kukaa kambi moja huku wakipatiwa mafunzo kutoka kwa Walimu wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo lengo likiwa ni kuwapika kisanaa na kuanza kushindanishwa ili kuweza kupata Mshindi mmoja ambaye ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane Jijini Dar Es Salaam.
Mara baada ya Fainali hiyo kumaliza washindi kumi watakaopatikana watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na wataweza kutengeneza filamu ya Pamoja na hatimaye kuja kunufaika na filamu hiyo.
Shindano la TMT limekuwa ni shindano kubwa kabisa ambalo halijawahi kufanyika nchini na limekuwa likirusha vipindi vyake katika kituo cha Runinga cha ITV kuanzia mida ya Saa Nne Usiku siku ya Jumamosi na Marudio yake ni Kila Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa 5 usiku huku Jumamosi ya tarehe 21 Juni 2014 kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa kupitia kituo hiko cha runinga na hatimaye Kazi ya Mchujo Kuanza Mara moja mara baada ya washindi wa kanda zote kuwasili Jijini Dar Es Salaam na kuanza kambi huku wananchi watakuwa wakiwapigia kura washiriki ambao wanawaona wenye uwezo.

No comments:

Post a Comment