Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman
Mbowe amemtunishia misuli, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema hawatishwi na
kusudio alilotoa la kubadili kanuni ili kudhibiti tabia ya kambi hiyo kususia
vikao vya Bunge kila wanapopinga hoja.Mbowe alisema jana mjini hapa kwamba,
wako tayari kwenda jela na hata ikibidi kufa kwa kupambana na ufisadi ndani ya
Serikali.
Pinda alitoa pendekezo hilo baada ya wabunge wa upinzani
ambao pia ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini na kutoka bungeni.(Martha Magessa).Baada ya
kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, Pinda alipendekeza kubadilishwa kwa
kanuni ili kuwadhibiti wabunge wa upinzani kutoka nje ya Bunge mara kwa mara."Inawezekana
kanuni zinaruhusu... lakini haiwezekani kila mnaposhindwa hoja muone njia
rahisi ni kutoka nje, nasema hivi, Watanzania hawawezi kukubaliana na
hili," alisema Pinda Ijumaa iliyopita na kuongeza:
"Tabia hii inayoendelea kujengeka siyo nzuri. Tuombe
kanuni za Bunge zirekebishwe kwa sababu Bunge linaonekana halina watu wakati
hao waliotoka hawana sababu za msingi."Akizungumzia pendekezo hilo, Mbowe
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema alisema wabunge wa kambi hiyo wako tayari
kupokea adhabu yoyote itakayotokana na kubadilishwa kwa kanuni za kudumu za
Bunge hilo.
"Katika kutafuta haki, ustawi na heri ya taifa letu na
ya vizazi vijavyo vya nchi yetu, tuko tayari siyo tu kukabili adhabu
zitakazotokana na kubadilishwa kwa kanuni, bali hata kwenda jela na kufa."Ni
heri kufa umesimama kwenye haki kuliko kuishi ukiwa umesimama kwenye ubatili.
Tunafahamu gharama na mateso tunayopitia kwa ajili ya
kupinga ufisadi na ubadhirifu. Tumeamua kupambana mpaka mwisho hatimaye haki na
ukweli vitatuweka huru."Baada ya kususia Bunge Ijumaa iliyopita, Mbowe
alikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa kulikuwa mkakati mahususi wa
kuwazomea na kuwatukana."Tulitambua kwamba kuna mkakati mkubwa
ulioandaliwa baina ya Serikali, uongozi wa Bunge na wabunge wa CCM kujaribu
kufukia ufisadi mkubwa ambao unaikumba ya Wizara ya Nishati na Madini,"
alisema Mbowe.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment