Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 6, 2014

MCHEZAJI NGULI WA SOKA GEBO PETER AFARIKI DUNIA

Marehemu  Gebo Peter(Kushoto) enzi za uhai wake.
Mshambuliaji wa zamani wa Sigara na Simba, Gebo Peter amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Beki wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya' amethibitisha taarifa za kifo hicho.
Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.
Kwa sasa, msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki, Dar es Salaam ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.
Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu.

No comments:

Post a Comment