Muhubiri wa kiisilamu ameuawa mjini mombasa pwani ya Kenya ,
ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni ya kiongozi mwingine wa kidini.
Sheikh Mohammed Idris, ambaye ni mwenyekiti wa baraza la
maimamu na wahubiri nchini Kenya, aliuawa karibu na msikiti ulio karibu na
nyumba yake na watu wasiojulikana.
Duru zinasema kwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana
wenye itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha
yake.
Wahubiri kadhaa mashuhuri wameuawa katika hali ya
kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na
kundi la wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa
mauaji yao, madai ambayo serikali imakenusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na
baadhi ya watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo
ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.
No comments:
Post a Comment