Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 10, 2014

MRADI WA UMEME VIJIJINI(REA)- TANESCO RUVUMA WAMEANZA KUSAMBAZA NGUZO VIJIJINI.

Wafanyakazi wa Tanesco wakishusha Nguzo za Umeme
Nguzo zikiwa zimeshushwa


Na Mpenda Mvula Songea


SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) Mkoani Ruvuma limeanza kusambaza nguzo kwa ajili ya Mradi wa Umeme Vijijini(REA) kama inavyoonekana pichani.
Nguzo hizo zimeanza kusambazwa katika Kijiji cha Masangu Kata ya Magagura Songea Vijijini Mkoani Ruvuma ambapo kwa Songea Vijijini Mradi huo unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu na kwa Mkoa mzima wa Ruvuma unatarajiwa kukamilika Julai Mwakani
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Francis Maze amesema 


kuwa hadi sasa zimeshasambazwa nguzo 1300 huku zikitarajiwa kusambazwa nguzo 12,000 kwa kwa Mkoa huo.
Amefafanua kuwa Nguzo hizo zimeanza kusambazwa Songea Vijijini katika Kata ya Magagura ili kuwezesha Umeme wa Mradi wa Tulila wa Maporomoko ya Maji unaotekelezwa na Watawa wa Chipole wa Kanisa Katoliki kuweza kupitisha umeme huo wa Megawati tano.

No comments:

Post a Comment